SWAHILI FASHION WEEK NA TUZO 2016 KUFUNGULIWA RASMI LEO

SWAHILI FASHION WEEK ITAFANYIKA TAREHE DESEMBA, 2,3 ,4 2016
Tarehe ya jukwaa kubwa la mtindo Afrika mashariki na kati Swahili Fashion Week 2016 yaliyopangwa kufanyika Desemba 2016 zimetolewa. Awamu ya Tisa ya Swahili Fashion Week (SFW16) itafanyika kuanzia Desemba 02-04, katika Makumbusho ya Taifa posta ambapo italeta pamoja zaidi ya wabunifu 40 kutoka Afrika mashariki na kwingineko, kushuhudia kwa dhati jukwaa hili bora la mitindo duniani
katika Kujenga mafanikio ya nguvu na ajabu ya misimu nane ya Swahili fashion week, jukwaa hili lina chukuliwa kuwa ni kiongozi katika katika suala la uvumbuzi na uoneshaji wa kazi za kibunifu. mwanzilishi wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali inatarajia kujenga msingi huu kwa shauku ya hali ya juu alisema, "si kwamba tu tulliionyesha dunia kuwa kina cha vipaji vya ubunifu nchini Tanzania na Afrika ni vya ajabu kweli, lakini sasa tuna vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali wanasubiri kuhudhuria na kuunga mkono jukwaa hili na kulikuza duniani kote. Kama mithali hii ya Afrika inavyosema “ kama unataka kwenda haraka nenda mwenyewe, kama unataka kwenda mbali nenda pamoja”
Mustafa aliongeza kuwa , "lengo la kuendeleza mtindo ya kiafrika bado lipo katika mstari wa mbele katika yale ambayo tumelenga kuyafanya, na kupitia kutanuka kwa jukwaa hili kutokana na vyombo mbali mbali vya habari, katika Tanzania, Afrika na kwengineko kwa ujumla zinaona kwamba kuna njia mbadala kwa bidhaa zetu kutoka nje, Tuna nia ya kukuza thamani ya bidhaa, kupigania dhana ya bidhaa zinazotangenezwa afrika na kujenga bidhaa zenye mizizi ya afrika "
toleo la tisa ya Swahili Fashion Week itaendelea kuwa kivutio katika maonesho yote ya wiki nchini afrika pamoja na wabunifu wa ndani, kikanda na kimataifa wakinyesha hisia zao za dhati. Mwaka huu tutakuwa na wabunifu 18 wa Kitanzania na 12 wabunifu wa kimataifa kuonyesha Jijini Dar es Salaam.

“tunaendelea kuwaomba jamii kukuza Tasnia ya ubunifu na kuvaa fahari ya vilivyo tengenezwa za Afrika hasa dhana ya Kitanzania. Vipaji vya ndani vinahitaji kulelewa na kuvihusisha bidhaa zinazotambulika ulimwenguni, kutoa ni moyo si utajiri, hivyo tunatazama mbele katika kuanza kuwasaidia kampuni ndogo ndogo na mashirika hili kuwezesha biashara hii ya mitindo ya ubunifu.” Lightness Kitua mratibu Swahili Fashion Week
Katika tukio hili la mwaka huu, mbali na maonyesho vya mavazi jukwaani unafanyika kila jioni kwa kipindi cha siku tatu kutoka 08:30 na kuendelea, na wakati mchana kutakuwa na tamasha la ununuzi wa bidhaa ambapo waonyeshaji mbalimbali watakuwa wakionyesha na kuuza kazi mbalimbali za mikono , sanaa na vifaa. Katika siku ya mwisho ya Desemba 4, maonesho yatasherekea maadhimisho ya sekta ya mitindo nchini kwa kutoa tuzo 24 kwa awshindi wataotangazwa usiku huu kupitia vipengele mbalimbali.

Swahili Fashion Week na tuzo 2016 ina ahidi kushinikiza teknolojia na kuonyesha uzalishaji wa juu na wa mwisho kabisa katika siku tatu za mtindo, uzuri, na mtindo wa maisha ya onesho hili na utembeaji wa kimataifa kutoka kwa wanamitindo na kuonyesha tamaduni mbali mbali zisizo sahaulika ambazo zinaendelea kuiweka Tanzania uangalizi wa kimataifa.
Swahili Fashion Week 2016 na Tuzo limeandaliwa na 361 degrees, kudhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Darling Hair, Colosseum Hotel & Spa, Tanzania Printers Ltd, Majira , Busines Times, Fabcars, Darlife, Asila’s Make up, Nexia Sj, Green telecom, A1outdoor, Epidor, Eventlites, Jumia Market, Michuz Blog , BASATA (Baraza La Sanaa La Taifa),
Fomu za Kupata kibali kwa waandishi wa habari, tafadhari sajili katika votuti vyetu ya www.swahilifashionweek.com

Share on Google Plus

About dr.joh health and wellness

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment