TUNGEONESHA VIPI UPENDO KWA WATU TUNAOWAPENDA
Kama ilivyo tuna siku 365 katika mwaka.inakuwaje ipo siku moja tu ya wapendanao? siku moja tu ya kuonesha upendo kwa watu tunaowapenda? Vipi kuhusu kuonesha jinsi gani tunawapenda watu kila siku ya maisha yetu?,yani siku zote 365? Is it possible? Inaweza kuwa ngumu lakini inabidi kujitahidi kuwaonesha jinsi gani tunawapenda wenzetu siku zote bila kujali uwepo wa Valentine's day..
wenyewe wanasema"Kila siku ni siku ya wapendanao kama upo kwenye mahusiano ya kweli"
NI LINI TUNGEPOKEA ROSES?
Siku hii utaona watu wakipeana maua waridi(roses) kuliko siku nyingine zote,kuna wenzangu na mimi siku hii tu ndo siku pekee tunapata maua kutoka kwa wapenzi wetu.
Kumsuprise mpenzi wako na maua au kitu chochote kizuri ni jambo ambalo linamfanya mtu kujiona ana thamani na kufeel upendo,,Kwa ambao wanafanyiwa hivi na wapenzi wao wanaelewa nachosema.Tuache utamaduni huu mbovu wa kusubiri valentines day ndo tupeleke maua kwa wapenzi wetu jamani.
JE NI LINI WAPENDANAO WANGEPASWA KUPEANA ZAWADI?
mwanzoni nilitangulia kusema kuwa tuna siku 365 katika mwaka,Guess what? unaweza kuchagua siku yoyote katika mwaka ukamsurprise mpenzi wako na bonge la zawadi na sio kusubiri tarehe 14 February.Fikiria kumpatia kipenzi chako zawadi siku yoyote katika mwaka.
SHUGHULI ZIPI TUNGEFANYA SIKU HII?
Good question... Tarehe 14 February isingekuwa valentines day ingekua siku tu ya kawaida kama siku nyingine,tungeendela na shughuli zetu za kila siku mfano kazi,biashara zatu na mambo mengine.Je tungeshindwa?
JE INGEKUWA VIGUMU?
Kutokana na jinsi watu tulivyozoea ingekua vigumu,lakini nachojaribu kusema hapa ni kwamba,Valentines day sio siku pekee ya kuonesha jinsi gani tunawapenda na kuwajali wapenzi wetu.Tusisite kuonesha upendo siku yoyote tu na sio kusubiri tarehe 14 February.
Una maoni gani kuhusu hili? Valentines day or not?
Blogger Comment
Facebook Comment